McEddy Elroy

Wednesday, August 8, 2012

HAPA TUNAFANYAJE BOSS?

Mhifadhi Ujirani mwema hifadhi ya Taifa ya Ruaha,Moronda Moronda ikiuliza jambo kwa Boss wake,Meneja Ujirani mwema kutoka TANAPA makao makuu,hivi karibuni kwenye moja ya mikutano ya ujirani mwema na wananchi huko Dodoma.


Thursday, August 2, 2012

NYUMBA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA

Nyumba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino,Mh.Gabriel Hoya,ipo kijiji cha Mpyayungu,kilomita 130 Magharibi mwa Mji wa Dodoma.

KARIBU NYAMA,PANDE MOJA TSH.1000

Mkazi wa kijiji cha Mpwayungu,Chamwino Mkoani Dodoma,akichoma nyama.

Naangalia Gari,sijawahi kuona!

Mtoto wa kijiji cha Chinugulu,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,akiangalia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo,Daudi Mayeji.Kijiji hicho ni nadra sana kufikiwa na magari mazito kama hili,kipo karibu kilomita 150 kutoka Dodoma mjini,kinapakana na pori tengefu la Lunda -Mkwambi.

CAMERA yako nzuri!

Watoto wa kijiji cha Manda,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,wakiangalia Camera yangu.Bila shaka ni mara yao ya kwanza kuona Camera kama hii.

NAFUNDISHA UJIRANI MWEMA!

Meneja wa Ujirani Mwema kutoka TANAPA Makao Makuu,Bw.Ahmed Mbugi akitoa mada juu ya mpango wa ujirani mwema kwa wananchi wa kijiji cha Manda,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hivi karibuni.

Moja ya vyoo vya wakazi wa kijiji cha Ilangali,tarafa ya Mpyayungu wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma