Friday, September 30, 2011

MTO RUAHA MKUBWA WABAKI MADIMBWI,HAKUNA MATUMAINI YA UMEME

Maji yanaendelea kuwa bidhaa nadra sana nchini.Hali ya Mto Ruaha Mkubwa (The Great Ruaha) ambao unategemewa sana na mabwawa yanayotumiwa na Shirika la Ugavi wa umeme nchini Tanzania (Tanesco) ya Mtera,Kidatu na Kihansi kuzalisha nishati hiyo, uko katika hali mbaya sana na kwa hakika hakuna matumaini kabisa kama mvua zitachelewa kunyesha.
Blog huu imetenbelea hifadhi ya ruaha wiki iliyopita na kufanikiwa kupata picha mbalimbali za mto huo hapo September 28,mwaka huu, zinaonesha namna hali ilivyo mbaya hali inayotishia ustawi wa hifadhi ya ruaha.
Historia ya hifadhi ya Ruaha haiwezi kutenganishwa na Mto Ruaha Mkuu au Mto Ruaha Mkubwa hivyo bila uwepo wa mto Ruaha Mkubwa, mimea na uoto mwingine wa asili utatoweka vivyo hivyo kwa wanyama ambao ni rasilimali kubwa ya Taifa la Tanzania.
Kwa sasa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kubwa kuliko hifadhi yoyote nchini ikiwa na meta za mraba 20,000 (Elfu ishirini).Ruaha pia ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika ikifuata kwa karibu kwa hifadhi ya Salonga iliyoko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya watu wa Congo.
Tutaendelea kukuletea habari hii kwa kina zaidi. Endelea kuwa nasi.

No comments:

Post a Comment