McEddy Elroy

Sunday, July 15, 2012


AFISA Wanyamapori Msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,Bwana Ramadhan Salum  anashikiliwa na Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Afisa huyo,anadaiwa kuua tembo wawili katika pori tengefu la Lunda-Mkwambi linalopakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa na kuuza nyama ya tembo hao kwa wananchi wa kijiji cha Chinugulu na hatimaye kukamatwa akiwa na meno ya Tembo hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino,Bwana Daudi Mayeji amethibitisha taarifa za Afisa wake kuua Tembo wawili na kisha kukamatwa na Polisi.
Kwa upande wake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Zelothe Stephen ameuabia ujumbe wa viongozi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha,TANAPA Makao makuu na kikosi dhidi ya ujangili kanda ya kati na nyanda za juu kusini uliotembelea ofisini kwake kuomba ushirikiano wa kukabiliana na ujangili kwamba, suala la ujangili sasa linahitaji hatua za haraka…INSERT
Meneja wa Ujirani Mwema wa TANAPA, Ahmed Mbungi na Mhifadhi ujirani mwema katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha,Bw.Moronda Moronda,wameomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya Afisa huyo wa wanyamapori ili kurejesha imani kwa wananchi.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha inapakana na vijiji 64 vilivyopo katika Mikoa mitatu ya Iringa,Mbeya na Dodoma na enaelezwa kuwa ujangili unaoongezeka kila kukicha unatishia ustawi wa hifadhi hiyo ya Ruaha..


Friday, July 13, 2012