AFISA Wanyamapori Msaidizi
wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,Bwana Ramadhan Salum anashikiliwa na Polisi Mkoani humo kwa tuhuma
za kujihusisha na ujangili.
Afisa huyo,anadaiwa kuua
tembo wawili katika pori tengefu la Lunda-Mkwambi linalopakana na hifadhi ya
Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa na kuuza nyama ya tembo hao kwa wananchi
wa kijiji cha Chinugulu na hatimaye kukamatwa akiwa na meno ya Tembo hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Chamwino,Bwana Daudi Mayeji amethibitisha taarifa za
Afisa wake kuua Tembo wawili na kisha kukamatwa na Polisi.
Kwa upande wake,Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma,Zelothe Stephen ameuabia ujumbe wa viongozi wa hifadhi ya
Taifa ya Ruaha,TANAPA Makao makuu na kikosi dhidi ya ujangili kanda ya kati na
nyanda za juu kusini uliotembelea ofisini kwake kuomba ushirikiano wa
kukabiliana na ujangili kwamba, suala la ujangili sasa linahitaji hatua za
haraka…INSERT
Meneja wa Ujirani Mwema wa
TANAPA, Ahmed Mbungi na Mhifadhi ujirani mwema katika hifadhi ya Taifa ya
Ruaha,Bw.Moronda Moronda,wameomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya Afisa huyo wa
wanyamapori ili kurejesha imani kwa wananchi.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
inapakana na vijiji 64 vilivyopo katika Mikoa mitatu ya Iringa,Mbeya na Dodoma
na enaelezwa kuwa ujangili unaoongezeka kila kukicha unatishia ustawi wa
hifadhi hiyo ya Ruaha..
No comments:
Post a Comment