McEddy Elroy

Thursday, August 2, 2012

Naangalia Gari,sijawahi kuona!

Mtoto wa kijiji cha Chinugulu,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,akiangalia gari la Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo,Daudi Mayeji.Kijiji hicho ni nadra sana kufikiwa na magari mazito kama hili,kipo karibu kilomita 150 kutoka Dodoma mjini,kinapakana na pori tengefu la Lunda -Mkwambi.

CAMERA yako nzuri!

Watoto wa kijiji cha Manda,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,wakiangalia Camera yangu.Bila shaka ni mara yao ya kwanza kuona Camera kama hii.

NAFUNDISHA UJIRANI MWEMA!

Meneja wa Ujirani Mwema kutoka TANAPA Makao Makuu,Bw.Ahmed Mbugi akitoa mada juu ya mpango wa ujirani mwema kwa wananchi wa kijiji cha Manda,wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hivi karibuni.

Moja ya vyoo vya wakazi wa kijiji cha Ilangali,tarafa ya Mpyayungu wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma

Sunday, July 15, 2012


AFISA Wanyamapori Msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma,Bwana Ramadhan Salum  anashikiliwa na Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Afisa huyo,anadaiwa kuua tembo wawili katika pori tengefu la Lunda-Mkwambi linalopakana na hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa na kuuza nyama ya tembo hao kwa wananchi wa kijiji cha Chinugulu na hatimaye kukamatwa akiwa na meno ya Tembo hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino,Bwana Daudi Mayeji amethibitisha taarifa za Afisa wake kuua Tembo wawili na kisha kukamatwa na Polisi.
Kwa upande wake,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Zelothe Stephen ameuabia ujumbe wa viongozi wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha,TANAPA Makao makuu na kikosi dhidi ya ujangili kanda ya kati na nyanda za juu kusini uliotembelea ofisini kwake kuomba ushirikiano wa kukabiliana na ujangili kwamba, suala la ujangili sasa linahitaji hatua za haraka…INSERT
Meneja wa Ujirani Mwema wa TANAPA, Ahmed Mbungi na Mhifadhi ujirani mwema katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha,Bw.Moronda Moronda,wameomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya Afisa huyo wa wanyamapori ili kurejesha imani kwa wananchi.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha inapakana na vijiji 64 vilivyopo katika Mikoa mitatu ya Iringa,Mbeya na Dodoma na enaelezwa kuwa ujangili unaoongezeka kila kukicha unatishia ustawi wa hifadhi hiyo ya Ruaha..


Friday, July 13, 2012